Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Claire O’Neill amejikuta akiungana kwa mara nyingine na mtoto wake wakike wa miezi minne baada ya wezi kuiba gari lake likiwa na mwanae huyo ndani
Claire O’Neill mwenye umri wa miaka 39, raia wa Uingereza alimuacha mtoto huyo kwenye gari lake aina ya ‘Audi A3 sports’ nje ya nyumba yake huko Birmingham kabla ya wezi kuliiba hapo jana siku ya Alhamisi majira ya mchana.
Wezi hao waliyokadiriwa kuwa wawili walikuwa wakimfuatilia mama huyo aliyekuwa amempakia mwanae kichanga anayejulikana kwa jina la Eliza kwenye siti za gari hiyo

